Share this
Tamthilia ya “Shackles of Doom” inajadili maudhui mbalimbali kama: ndoa ya lazima, ubakaji, hali duni ya kazi na mengine pamoja na ule maudhui kuu ya ukabila.
Sanaa ni kioo cha jamii – kumaanisha yale tunayoyaona katika tamthilia hiki ni kigezo cha yale yanayoendelea katika jamii zetu na siyo mashtaka dhidi ya jamii fulani humu nchini kama ilivyo chukuliwa na watu wengi.
Mambo kama ndoa ya lazima ama za kupangwa ni mambo ambayo tumeyaona hata baina ya jamii yetu wenyewe hata na marafiki. Tumeona jamii wakiozana ili kukuza hadhi yao ya kiuchumi.
Lakini pia ni muhimu tuchukue funzo kutoka kwa sanaa kama haya na kujiepusha na vitendo ambavyo huenda yangatenganisha jamii kama ugavi wa rasilmali ya uma kwa njia isiyofaa.
Si mara ya kwanza kuona jamii wenye ardhi wakibaguliwa katika ajira inayotokana na kupatikana kwa maadini fulani ama kuanzinshwa kwa kiwanda fulani katika ardhi yao.
Fauka ya hayo, mambo kama ndoa ya kulazimishwa na ubakaji katika familia ni mambo ambayo lazima tuyakatae na kuhakikisha kwamba yamesitishwa katika jamii yetu.
Follow me on twitter @IamOminde